Page 88 - SayansiStd4
P. 88
Jaribio namba 2: Kuchunguza vipitisha joto vizuri na
vipitisha joto hafifu
Lengo: Kutambua vipitisha joto vizuri na vipitisha joto
FOR ONLINE READING ONLY
hafifu kupitia vitu yabisi
Mahitaji: Kijiko cha chuma, kijiko cha plastiki, kijiti cha
mbao, kikombe chenye maji ya moto na vipande
vidogo vya siagi
Tahadhari: Usimamizi wa mwalimu unahitajika.
Hatua
1. Weka kipande kidogo cha siagi kwenye ncha ya kijiko cha
chuma, kijiko cha plastiki na kijiti cha mbao. Hakikisha
siagi inashika vizuri kwenye ncha ya kila kifaa.
2. Zamisha sehemu ya chini ya kila kijiko na kijiti cha mbao
(sehemu isiyo na siagi) kwenye maji ya moto kwa wakati
mmoja.
3. Chunguza ni kipande gani cha siagi kitayeyuka haraka
na andika matokeo ya kile kilichotokea.
Matokeo
Kijiko cha chuma kimesafirisha joto haraka kutoka kwenye maji
ya moto, na kusababisha siagi kuyeyuka kwa haraka. Kifaa
ambacho siagi yake imeyeyuka kwa haraka ni kipitishi kizuri
cha joto. Kijiko cha plastiki na kijiti cha mbao vimesafirisha
joto kwa polepole zaidi na siagi inaweza kuchukua muda
mrefu kuyeyuka au kutoyeyuka kabisa. Kifaa ambacho siagi
yake imechelewa kuyeyuka au kutoyeyuka kabisa ni kipitishi
hafifu cha joto.
81
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 81
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 81 14/01/2025 18:39