Page 87 - SayansiStd4
P. 87
Hatua
1. Laza kipande cha metali juu ya kipande cha ubao.
Angalia Kielelezo namba 2(a).
FOR ONLINE READING ONLY
2. Weka nta au mshumaa katika ncha moja ya kipande cha
metali angalia kielelezo namba 2(b).
3. Weka kipande cha karatasi ngumu au ya boksi kati ya
nta na ubao ili huzuia nta kupata joto moja kwa moja
kutoka kwenye jiko. Angalia Kielelezo namba 2(c).
4. Weka jiko katika ncha ya upande mwingine wa kipande
cha metali. Angalia Kielelezo namba 2(c).
Kielelezo namba 2: Kusafiri kwa joto kwenye vitu yabisi
5. Washa jiko, kisha subiri. Je, nini kinatokea kwenye nta?
6. Andika matokeo ya kile kilichotokea kwenye nta baada
ya kuwasha moto.
Matokeo
Baada ya kuwasha jiko, nta iliyeyuka. Hii inaonesha kuwa
joto lilisafiri kutoka kwenye chanzo, kipande cha metali hadi
kwenye nta.
Hitimisho
Jaribio hili linathibitisha kuwa joto husafiri katika maada yabisi
kwa njia ya mpitisho.
80
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 80
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 80 14/01/2025 18:39