Page 84 - SayansiStd4
P. 84
Sura ya Tano
Nishati
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Kuna nishati mbalimbali zinazotumika katika maisha ya kila
siku. Katika sura hii, utajifunza aina na matumizi ya nishati ya
joto, mwanga na sauti. Vilevile, utafanya majaribio sahili ya
baadhi ya aina za nishati. Umahiri utakaoujenga utakusaidia
kubaini vyanzo vya nishati na kutumia nishati kwa ufanisi
katika maisha ya kila siku.
Fikiri Maisha yangekuwaje bila nishati.
Maana ya nishati
Katika mazingira tunayoishi kuna vyanzo mbalimbali vya nishati.
Nishati hizi zina uwezo wa kusababisha kazi kufanyika. Hivyo,
nishati ni uwezo unaowezesha kazi mbalimbali kufanyika.
Aina za nishati
Kuna aina mbalimbali za nishati tunazotumia katika maisha ya
kila siku. Baadhi ya nishati hizo ni kama vile nishati ya joto,
mwanga na sauti.
Nishati ya joto
Joto ni aina ya nishati inayosafiri kati ya vitu vyenye jotoridi
tofauti. Joto hutokana na vyanzo vya asili kama vile nyota
77
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 77
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 77 14/01/2025 18:39