Page 89 - SayansiStd4
P. 89
Hitimisho
Jaribio hili limebainisha jinsi yabisi tofauti kama vile chuma,
plastiki na mbao zinavyopitisha joto. Hivyo, kutuwezesha
FOR ONLINE READING ONLY
kutofautisha kati ya vipitishi joto vizuri na hafifu.
Jaribio namba 3: Kuchunguza joto linavyosafiri katika
vimiminika
Lengo: Kuonesha kusafiri kwa joto katika vimiminika
Mahitaji : Sufuria, jiko, kibiriti, maji, vipande vidogo vya
karatasi ya A na kipimajoto
4
Tahadhari: Chukua tahadhari wakati wote wa jaribio ili
usipate madhara ya moto.
Hatua
1. Chukua vipande vidogo vya karatasi na tumbukiza katika
sufuria.
2. Weka maji baridi ndani ya sufuria na acha kwa muda
wa dakika tano. Je, nini kimetokea kwenye vipande vya
karatasi? Angalia Kielelezo namba 3(a).
3. Pima maji hayo kwa kutumia kipimajoto, kisha rekodi.
4. Bandika sufuria yenye vipande vya karatasi na maji
kwenye jiko linalowaka kama inavyoonekana kwenye
Kielelezo namba 3(b).
5. Subiria kwa dakika kumi, kisha pima jotoridi la maji hayo
kwa kutumia kipimajoto na urekodi.
82
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 82
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 82 14/01/2025 18:39