Page 94 - SayansiStd4
P. 94
Picha Maelezo
FOR ONLINE READING ONLY
Kunyoosha nguo kwa lengo la
kuuwa vijidudu na kufanya nguo
kuwa nadhifu.
Kukausha mazao ili kuondoa
unyevu ambao unaweza
kusababisha mazao kuharibika.
Matumizi mengine ya joto ni kupika chakula, kuchemsha maji
ya kunywa, kuyeyusha vyuma viwandani na kuzalisha umeme.
Vilevile, joto hutumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali
kama vile metali, plastiki na glasi.
Zoezi
Sehemu A: Andika KWELI kwa sentensi sahihi na SI KWELI
kwa sentensi isiyo sahihi.
1. Kuni, mkaa, makaa ya mawe na gesi ni vyanzo vya joto
visivyo vya asili.
2. Chuma na ubao ni rahisi kupitisha joto.
3. Joto linaweza kusafiri katika vitu vyenye hali ya yabisi,
kimiminika na gesi.
4. Tunakausha mazao kwa kutumia nishati ya joto.
5. Joto na jotoridi ni vitu vyenye maana moja.
87
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 87
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 87 14/01/2025 18:39