Page 96 - SayansiStd4
P. 96
Kazi ya kufanya namba 2
Tumia vyanzo mbalimbali vya taarifa ikiwemo maktaba
mtandao, video za kielektroniki na maabara za kidijitali
FOR ONLINE READING ONLY
kufanya kazi hii.
1. Orodhesha mifano ya vyanzo vya nishati ya mwanga
vilivyo katika mazingira yako.
2. Chora mifano hiyo ulivyoorodhesha kwenye namba 1
hapo juu na andika matumizi ya kila kimoja.
Mifano ya vyanzo vya nishati ya mwanga ni kama vile jua, taa
na tochi. Jua husaidia mimea kukua, taa husaidia kusoma na
tochi husaidia kuona gizani.
Vitu vinavyoruhusu na visivyoruhusu mwanga kupenya
Kazi ya kufanya namba 3
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine vya
taarifa kubaini vitu vinavyopitisha mwanga, visivyopitisha
mwanga au vinavyopitisha mwanga kiasi.
2. Kwa kutumia taarifa za sehemu (a), chunguza vitu katika
Jedwali namba 3 kisha weka alama “√” panapohusika.
Jedwali namba 3: Vitu vinavyoruhusu au visivyoruhusu
mwanga
Inaruhusu Hairuhusu Inaruhusu
Picha mwanga mwanga mwanga kiasi
(Angavu) (Kinzanuru) (Nusuangavu)
Kipande cha barafu
89
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 89 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 89