Page 99 - SayansiStd4
P. 99
3. Mulika kitabu kwa kurunzi, kisha andika matokeo
uliyoyaona.
4. Rudia hatua ya tatu kwa vifaa vingine vilivyotajwa hapo
juu.
FOR ONLINE READING ONLY
5. Andika matokeo ya kila kimoja kadiri ulivyoona kwa
kuzingatia maelekezo haya:
(a) Je, ni vitu vipi vilivyoruhusu miale ya mwanga kupenya?
(b) Je, ni vitu vipi havikuruhusu miale ya mwanga
kupenya?
(c) Je, nini kimetokea mwanga ulipotua juu ya nyuso za
vitu hivyo?
Matokeo
Glasi tupu na miwani vinaruhusu mwanga kupita. Kikombe
cheusi cha plastiki, kipande cha ubao na kitabu, haviruhusu
mwanga kupita. Kitambaa cheupe na glasi iliyojaa maji
vinaruhusu mwanga kiasi kupita.
Hitimisho
Vitu angavu vinaruhusu mwanga kupita. Vitu nusuangavu
vinaruhusu mwanga kiasi kupita na vitu kinzanuru haviruhusu
mwanga kupita.
Jaribio namba 6: Kuchunguza kusafiri kwa mwanga kwenye
mstari mnyoofu
Lengo: Kuonesha mwanga unavyosafiri katika mstari
mnyoofu
Mahitaji: Glasi yenye maji, karatasi ngumu isiyo pitisha
mwanga, karatasi ngumu yenye tobo, kurunzi na
maji
92
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 92
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 92 14/01/2025 18:39