Page 104 - SayansiStd4
P. 104
Kuakisiwa kwa miale ya mwanga
Kuakisiwa kwa mwanga ni kitendo
cha kurudishwa kwa miale ya
mwanga inapotua kwenye sura
FOR ONLINE READING ONLY
nyororo na inayong’aa. Mfano
wa kifaa chenye sura nyororo na
inayong’aa ni kioo bapa. Chunguza
Kielelezo namba 11, kisha fanya
kazi inayofuata.
Kielelezo namba 11:
Kutokea kwa taswira katika
kioo bapa
Kazi ya kufanya namba 5
Kuchunguza kuakisiwa kwa mwanga
Mahitaji: Kioo bapa, meza na kalamu
Hatua
1. Chukua kioo bapa, kisimamishe kwenye meza, kisha
jiangalie kwenye kioo.
2. Chukua kalamu, isimamishe mbele ya kioo.
3. Andika matokeo ya vitendo ulivyofanya. Je, umegundua
nini kutokana na uchunguzi ulioufanya?
Miale ya mwanga inapotua katika uso nyororo unaong’aa
huakisiwa. Kuakisiwa kwa miale ya mwanga husababisha
kutengenezwa kwa taswira ya kitu au mtu kwenye kioo. Chukua
mfano wa kujiona kwenye kioo. Unapojiangalia kwenye kioo,
mwanga kutoka kwenye chanzo hugonga mwili wako na kurudi
kwenye kioo, kioo huakisi mwanga huo na kurudi machoni
mwako na kuwezesha kuona taswira yako.
97
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 97 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 97