Page 105 - SayansiStd4
P. 105
Kupinda kwa miale ya mwanga
Sifa nyingine ya mwanga ni kupinda kwa miale ya mwanga.
Miale ya mwanga hupinda inapotoka midia moja angavu kwenda
midia nyingine angavu. Kwa mfano, kutoka kwenye midia ya
FOR ONLINE READING ONLY
hewa kwenda midia ya maji. Kwa hiyo, mwanga utapita kwenye
hewa kwenda kwenye maji, miale ya mwanga huo hupinda.
Hatuoni miale ya mwanga ikipinda bali tunaona matokeo ya
kupinda kwa miale ya mwanga. Chunguza Kielelezo namba
12, kisha fanya jaribio linalofuata.
Kielelezo namba 12: Matokeo ya kupinda kwa miale ya mwanga
Jaribio namba 8: Kuchunguza kupinda kwa miale ya
mwanga
Lengo: Kuonesha miale ya mwanga inavyopinda
Mahitaji: Bakuli angavu au bika, maji safi ndani ya jagi na
penseli
98
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 98 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 98