Page 100 - SayansiStd4
P. 100
Hatua
1. Weka glasi iliyojaa maji juu ya dawati.
2. Weka karatasi isiyopitisha mwanga yenye tobo mbele ya
glasi.
FOR ONLINE READING ONLY
3. Weka karatasi isiyo na tobo upande wa pili wa glasi.
4. Elekeza mwanga wa kurunzi kwenye tobo kama
inavyooneshwa katika Kielelezo namba 7. Je, unaweza
kuona mwanga wa kurunzi katika karatasi ngumu isiyo na
tobo? Andika matokeo ya uchunguzi.
Kielelezo namba 7: Mwanga unavyosafiri
5. Ondoa glasi yenye maji kisha weka karatasi isiyopitisha
mwanga yenye tobo. Hakikisha iwe kwenye mpangilio
kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 7. Andika
matokeo ya uchunguzi.
6. Sogeza kidogo karatasi isiyopitisha mwanga yenye tobo.
Hakikisha umebadili mpangilio wa njia ya mwali. Andika
matokeo ya uchunguzi.
Matokeo
Miale ya mwanga imetoka kwenye kurunzi na kupita kwenye
tobo. Kisha, miale hiyo imepita kwenye maji na glasi na kutoka
nje hadi kwenye karatasi isiyo na tobo. Kubadili mpangilio wa
njia ya mwali kumezuia mwanga kupita
93
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 93
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 93 14/01/2025 18:39