Page 101 - SayansiStd4
P. 101
Hitimisho
Hii inaonesha kuwa, mwanga husafiri katika mstari mnyoofu.
FOR ONLINE READING ONLY
Sifa za mwanga
Sifa za mwanga ni kusafiri katika mstari mnyoofu, kutengeneza
kivuli, kupinda na kuakisiwa.
Kazi ya kufanya namba 4
Kuchunguza mwanga unavyosafiri katika hewa
1. Chunguza asubuhi na mapema jua linapochomoza. Je,
unaona nini?
2. Weka kumbukumbu ya kile unachokiona.
Ukiamka asubuhi na mapema wakati jua linaanza kuchomoza
utaona miale ya mwanga. Miale hii huonekana inasafiri
katika mistari iliyonyooka. Mwanga unatuwezesha kuona vitu
mbalimbali. Angalia Kielelezo namba 8 kinachoonesha namna
mwanga unavyosaidia kuona vitu mbalimbali.
Kielelezo namba 8: Mwanga unatusaidia kuona vitu mbalimbali
94
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 94 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 94