Page 106 - SayansiStd4
P. 106
Hatua
1. Chukua bakuli angavu lililo tupu au bika. Tumbukiza
sehemu ya penseli ndani ya bakuli hilo ukiwa umeishikilia.
2. Chunguza jinsi penseli inavyoonekana.
FOR ONLINE READING ONLY
3. Mimina maji kutoka kwenye jagi mpaka yafike nusu ya
bakuli au bika kama inavyoonekana kwenye Kielelezo
namba 12.
4. Chunguza tena mwonekano wa penseli iliyopo ndani ya
bakuli au bika baada ya kuweka maji. Je, kuna tofauti
gani kwenye mwonekano wa penseli kabla na baada ya
kumimina maji?
Matokeo
Penseli inaonekana imepinda kutokana na miale ya mwanga
kupinda
Hitimisho
Jaribio linathibitisha kwamba miale ya mwanga hupinda
inapopita kwenye midia angavu tofauti.
Matumizi ya nishati ya mwanga
Mwanga hutumika katika mambo mbalimbali kama
inavyooneshwa kwenye Jedwali namba 4.
Jedwali namba 4: Matumizi ya nishati ya mwanga
Picha Maelekezo
Kuona: Mwanga hutusaidia
kuona vitu. Bila mwanga,
hatungeweza kuona rangi,
maumbo, au vitu vilivyo karibu
nasi.
99
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 99
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 99 14/01/2025 18:39