Page 107 - SayansiStd4
P. 107
Picha Maelekezo
Fotosinthesisi: Mimea
FOR ONLINE READING ONLY
hutumia mwanga kutoka jua
kutengeneza chakula chao.
Mchakato huu husaidia mimea
kukua na kuwa na afya.
Paneli za sola: Paneli za sola
huchukua mwanga wa jua
na kubadilisha kuwa umeme,
ambao unaweza kutumika
nyumbani.
Lenzi (glasi za kukuzia): Lenzi
hutumia mwanga kufanya vitu
kuonekana vikubwa na wazi
zaidi.
Kurunzi: Kurunzi hutumia
mwanga kutusaidia kuona
gizani.
Nishati ya sauti
Sauti ni aina ya nishati ambayo tunaweza kuisikia. Sauti
hutokana na mitetemo ya vitu mbalimbali. Nishati hii husambaa
kutoka kwenye chanzo kwenda sehemu nyingine kwa kwenda
mbele na kurudi nyuma. Unapopiga ngoma, filimbi au gitaa,
kinachotokea ni sauti. Vilevile, vyanzo vingine vya sauti ni
100
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 100
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 100 14/01/2025 18:39