Page 112 - SayansiStd4
P. 112
Hatua
1. Chukua kipande kirefu cha chuma na kiweke mezani kama
Kielelezo namba 16 kinavoonesha.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 16: Kusafiri kwa sauti kwenye chuma
2. Mwambie rafiki yako aweke sikio lake kwenye upande
mmoja wa kipande hicho.
3. Gonga kipande cha chuma kwa kutumia rula.
4. Muulize anasikia nini na uandike.
5. Weka sikio lako upande mmoja wa chuma.
6. Mwambie rafiki yako agonge chuma upande mwingine wa
chuma.
7. Andika unachokisikia.
Vitu kama vile chuma, maji na hewa hupitisha sauti. Hii
inaonesha kuwa baadhi ya vitu yabisi, vimiminika na hewa
husafirisha sauti.
105
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 105
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 105 14/01/2025 18:39