Page 111 - SayansiStd4
P. 111
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 15: Kusafiri kwa sauti katika maji
Hatua
1. Chukua ndoo na ijaze maji.
2. Chukua kengele na itumbukize ndani ya maji ukiwa
umeishikilia kwa mkono mmoja bila kuiachia.
3. Sogeza sikio lako karibu na maji yalikoishia, lakini hakikisha
maji hayaingii sikioni.
4. Gonga kengele ndani ya maji kama Kielelezo namba 15
kinavyoonesha
5. Je, unasikia nini? Andika matokeo.
Sauti husafiri katika maji kama ilivyo katika hewa ingawa sauti
husafiri kwa haraka katika maji. Unapogonga kengele ndani ya
maji sauti husikika. Hii inaonesha jinsi sauti inavyosafiri katika
maji.
Kazi ya kufanya namba 9
Kuchunguza sauti inavyosafiri kupitia chuma
Mahitaji: Kipande kirefu cha chuma, meza na rula
104
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 104
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 104 14/01/2025 18:39