Page 113 - SayansiStd4
P. 113
Kazi ya kufanya namba 10
Pitia makala mtandao au video mtandao, kisha elezea kwa
FOR ONLINE READING ONLY
kifupi ni midia ipi kati ya hewa, maji na yabisi husafirisha sauti
kwa kasi zaidi.
Matumizi ya nishati ya sauti
Nishati ya sauti hutumika kwa mawasiliano katika sehemu
mbalimbali kama vile nyumbani, shuleni na barabarani. Vyombo
vya mawasiliano kama vile simu, tableti, radio, televisheni na
kompyuta hutoa sauti kuwezesha kuwasiliana. Vyombo hivi
hutupatia habari, burudani na taarifa mbalimbali kwa kutumia
sauti au sauti na picha tembezi.
Sauti pia hutumika katika matibabu. Kwa mfano, vifaatiba
mbalimbali hutumia nishati ya sauti kufanya vipimo mbalimbali
pamoja na upasuaji, kama ilivyo katika Kielelezo namba 17 (a)
Ambulensi ina king’ora ambacho hutumia nishati ya sauti kutoa
tahadhari ya dharura ya kimatibabu. Angalia Kielelezo namba
17 (b).
(a) Nishati ya sauti kwenye kifaatiba (b) Nishati ya sauti kwenye
ambulensi
Kielelezo namba 17: Baadhi ya vifaa vinavyotumia nishati ya sauti
106
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 106
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 106 14/01/2025 18:39