Page 118 - SayansiStd4
P. 118
Sehemu D: Maswali ya majibu mafupi
16. Taja vitu viwili vinavyoruhusu mwanga kupita.
17. Eleza jinsi kivuli kinavyotokea.
FOR ONLINE READING ONLY
18. Unapoimba wimbo nishati ipi hutokea?
19. Fafanua njia kuu tatu za kusafiri kwa joto.
20. Kuku huatamia mayai yake ili kuyapatia nishati gani?
21. Kuna tofauti gani kati ya nyuso za vitu vinavyoakisi na
visivyoakisi mwanga?
22. Nini hutokea mwale wa mwanga unaposafiri kutoka midia
moja angavu kwenda nyingine?
Msamiati
Akisi rudisha miale ya mwanga kutoka kwenye
kitu chenye sura nyororo na inayong’aa
Ambulensi gari maalumu lililowezeshwa kuchukua
wagonjwa au watu waliojeruhiwa haraka
kwenda au kutoka hospitali
Atamia hali ya ndege kulalia mayai yake
Egemeo kitu kinachosaidia kingine kusimama au
kujitegemea
Fikicha weka katikati ya vidole au viganja viwili na
kusugua
Kandili taa ya chemli inayowaka kwa utambi na
mafuta
Kioevu kimiminika kilicho katika hali ya majimaji
Midia hali ya mahali au kitu yabisi, kimiminika au
gesi ambapo mwanga hupita
Ombwe nafsi tupu
111
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 111
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 111 14/01/2025 18:39