Page 119 - SayansiStd4
P. 119
Sura ya Sita
Usimbaji katika kompyuta
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Kompyuta zinatusaidia kufanya mambo mengi katika
maisha yetu ya kila siku. Katika sura hii, utajifunza kuchora
maumbo yanayoweza kutumika katika maisha ya kila siku.
Pia, utajifunza kupangilia maumbo kimantiki ili kutengeneza
miundo. Vilevile, utajifunza kuunda michezo sahili kwa
kutumia program ya Scratch. Umahiri utakaoujenga
utakuwezesha kufikiri kimantiki na kuandaa michezo sahili
ya kompyuta..
Kazi mbalimbali zinazoweza kufanywa
Fikiri
kwa kutumia kompyuta
Dhana ya Miundo
Miundo ipo katika kila mahali tunapoishi. Muundo ni kitu
ambacho kimepangwa kwa mpangilio wa kimantiki ambao
hufanya iwe rahisi kutabiri kipengele kinachofuata katika
mfuatano. Baadhi ya miundo ni ya asili kama vile mistari ya
pundamilia na mingine ni ya kutengenezwa kama vile ubao wa
drafti, angalia Kielelezo namba 1.
112
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 112
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 112 14/01/2025 18:39