Page 109 - SayansiStd4
P. 109
Sauti inapotengenezwa, chembe za hewa hutetema na
kugongana. Hali hii, husababisha mitetemo ambayo hutoa
mawimbi ya sauti. Tunaweza kusema kuwa mawimbi ya sauti
husambaa kwa mitetemo ya vitu. Vitu hivi husafirisha sauti
FOR ONLINE READING ONLY
kwa kutetemesha chembechembe. Kwa mfano, ndege ya
abiria inaweza kuwa mbali angani, lakini sauti husikika kwa
kutetemesha molekuli za hewa kutoka kwenye ndege kwenda
sikioni. Sauti inasafirishwa kutoka kwenye ndege hadi kwenye
sikio kupitia hewa.
Kuakisiwa kwa sauti
Sauti iliyoakisiwa huitwa mwangwi. Mwangwi hutokea wakati
mawimbi ya sauti yanapogonga kutoka kwenye uso wa vitu na
kurudi kwa msikilizaji. Hali hii hutokea sehemu ambazo mawimbi
ya sauti hukutana na vitu vinavyoakisi sauti. Mfano wa vitu
vinavyoakisi sauti ni ukuta au vitu vikubwa. Muda ambao sauti
huchukua mpaka kurudi kwa msikilizaji husaidia kupata umbali
wa kiliko kitu kilichoakisi.
Kazi ya kufanya namba 7
Kufanya kitendo cha kutoa mwangwi
1. Ingia kwenye ukumbi usio na kitu, kisha simama angalau
umbali wa mita 17 kutoka kwenye moja ya ukuta kama
Kielelezo namba 14 kinavyoonesha.
2. Ita kwa sauti kubwa. Je, unasikia nini?
3. Andika matokeo ya kitendo ulichofanya.
102
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 102
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 102 14/01/2025 18:39