Page 110 - SayansiStd4
P. 110
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 14: Kuonyesha mwangwi unavyotokea
Uliposimama kwenye ukumbi mtupu na kuita kwa sauti kubwa,
ulisikia sauti ikijirudia. Kwa mfano, ukisema “hello” baada
ya dakika chache utasikia neno “hello” tena. Sauti hii huitwa
mwangwi. Kilichotokea ni mawimbi ya sauti yalitoka kwenye
mdomo wako na kusafiri kwenye hewa ndani ya ukumbi,
ikagonga ukuta mtupu na kurudi tena na kusababisha wewe
kusikia sauti uliyoita. Sauti inapokutana na kizuizi au kitu
kigumu kama ukuta au mwamba huakisiwa.
Kusafiri kwa sauti katika maada
Kazi ya kufanya namba 8
Kuchunguza sauti inavyosafiri katika maji
Mahitaji: Ndoo, maji na kengele au kitu chochote kinachoweza
kutoa sauti
103
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 103
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 103 14/01/2025 18:39