Page 102 - SayansiStd4
P. 102
Jaribio namba 7: Kuchunguza kivuli kinavyotokea
FOR ONLINE READING ONLY
Lengo: Kuonesha kivuli kinavyotokea
Mahitaji: Mpira, kurunzi, kikombe, kiti, mwanga wa jua
kifaa cha kutegemeza kama stuli na meza
Hatua
1. Shika mkononi kikombe au kitabu kuelekea kwenye
mwanga wa jua. Je, unaona nini?
2. Weka meza na kiti nje ya darasa kwenye mwanga wa jua.
3. Angalia chini ya meza na kiti. Je, unaona nini?
4. Ingia kwenye chumba chenye giza. Weka mpira juu ya
egemeo, kisha washa kurunzi ukielekeza kwenye mpira
kama ilivyooneshwa katika Kielelezo namba 9. Je, unaona
nini?
5. Andika matokeo ya unachokiona katika hatua ya 1, 3 na 4.
Kielelezo namba 9: Tochi iliyowaka kuelekea kwenye mpira na kivuli
kutokea ukutani
95
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 95
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 95 14/01/2025 18:39