Page 98 - SayansiStd4
P. 98
Katika mazingira tunayoshi, baadhi ya vitu huruhusu miale
ya mwanga kupenya. Vitu hivyo huitwa angavu. Kwa mfano,
glasi na baadhi ya plastiki. Vitu vingine huruhusu kiasi cha
mwanga kupenya vitu hivyo huitwa nusuangavu. Kwa mfano,
FOR ONLINE READING ONLY
chupa yenye ukungu. Pia, vitu visivyopitisha mwanga huitwa
vikinzanuru. Kwa mfano, ubao, kitabu na kuta.
Kutokana na vyanzo vya taarifa ulivyopitia umeona jinsi mwanga
unavyopita katika vitu mbalimbali. Kwa kuweka alama ya “√”
kwenye mchoro, inaonesha kuwa:
(a) Mwanga hupita kwa urahisi katika vitu angavu, kwa mfano,
kioo cha mbele cha gari, dirisha la kioo na bakuli la kioo.
(b) Mwanga unapita kiasi tu katika vitu nusuangavu, kwa
mfano, kioo kilichofunikwa na ukungu na kipande cha
barafu.
(c) Mwanga hauwezi kupenya kwenye vikinzanuru. Kwa
mfano, kipande cha ubao na sufuria.
Jaribio namba 5: Kuchunguza kupenya kwa mwanga katika
vitu
Lengo: Kuonesha uwezo wa vitu mbalimbali kupitisha
mwanga
Mahitaji: Kurunzi, betri, glasi tupu, kikombe cha plastiki cha
rangi nyeusi, kitambaa cheupe, miwani, kipande
cha ubao, glasi iliyojaa maji na kitabu
Hatua
1. Chukua kurunzi, weka betri, washa ili uone ikitoa mwanga.
2. Ingia kwenye chumba chenye giza ukiwa na kurunzi
uliyoiwasha. Panga vitu vilivyotajwa juu ya meza.
91
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 91
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 91 14/01/2025 18:39