Page 95 - SayansiStd4
P. 95
Sehemu B: Maswali ya majibu mafupi
6. Taja vitu vitatu vinavyopitisha joto.
7. Eleza umuhimu wa nishati ya joto katika matumizi ya
FOR ONLINE READING ONLY
nyumbani.
8. Eleza, kwa nini mkono wa sufuria au pasi hutengenezwa
kwa plastiki au mti?
9. Kwa nini kipindi cha masika baadhi ya nguo huchelewa
kukauka?
10. Kwa nini tunashauriwa kuvaa sweta na kujifunika blanketi
wakati wa baridi?
Nishati ya mwanga
Nishati ya mwanga ni aina mojawapo ya mionzi ya
sumakuumeme. Kuna aina kuu mbili za vyanzo vya nishati
ya mwanga ambavyo ni vyanzo vya asili na visivyo vya asili.
Mifano ya vyanzo vya asili ni nyota ikijumuisha jua, radi na
viumbe wenye mwanga wa kibaiolojia. Kwa upande mwingine
vyanzo visivyo vya asili ni kama vile moto, tochi, mshumaa na
fataki. Kielelezo namba 6 kinaonesha vyanzo vya nishati ya
mwanga.
(a) Taa ya chemli (b) Jua (c) Balbu (c) Tochi
Kielelezo namba 6: Vyanzo vya nishati ya mwanga
88
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 88
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 88 14/01/2025 18:39