Page 91 - SayansiStd4
P. 91
Baada ya sufuria yenye maji na vipande vya karatasi kupata
joto, maji yaliyo na joto yalipanda juu pamoja na vipande vya
karatasi. Vilevile, jotoridi la maji lilionekana kupanda baada
ya kuyachemsha. Hii inamaanisha joto lilisafiri kutoka kwenye
FOR ONLINE READING ONLY
jiko kupitia sufuria mpaka kwenye maji kwa njia ya msafara.
Hitimisho
Katika jaribio hili, tumeona kuwa maji yakipata joto hupanda
juu na kusafirisha joto kwa njia ya msafara.
Jaribio namba 4: Kuchunguza joto linavyosafiri katika nafasi
tupu
Lengo: Kuonesha kusafiri kwa joto katika nafasi tupu
Mahitaji: Kitambaa, maji, kamba ya kuanikia nguo,
vibanio na beseni
Hatua
1. Weka maji katika beseni.
2. Chukua kitambaa kikavu, kisha kiweke ndani ya maji.
Je, kitambaa kinaonekanaje?
3. Ondoa kitambaa katika beseni. Kamua kidogo na,
kisha, kianike juani kwa muda wa saa moja kama
inavyoonekana kwenye Kielelezo namba 4.
4. Baada ya saa moja ondoa kitambaa na kichunguze. Je,
kitambaa kinaonekanaje?
84
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 84
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 84 14/01/2025 18:39