Page 86 - SayansiStd4
P. 86
2. Andika unachohisi wakati wa kufikicha viganja vya
mikono yako.
3. Chukua kijiti chembamba kilichokauka.
FOR ONLINE READING ONLY
4. Pekecha kijiti kwenye kipande cha mti uliokauka.
5. Gusa sehemu ya kijiti iliyopekechwa na andika matokeo.
Vipo vyanzo mbalimbali vya joto kama vile jua, umeme, kuni
zinazowaka na msuguano. Pia, baadhi ya aina za nishati
zinaweza kubadilishwa ili kutoa nishati ya joto. Kwa mfano,
mwanga wa jua hubadilishwa kuwa nishati ya joto, umeme na
kemikali. Vilevile, msuguano baina ya vitu viwili hutoa nishati
ya joto kama ulivyobaini kwenye Kazi ya kufanya namba 1.
Kusafiri kwa joto
Nishati ya joto inaweza kusafiri kutoka kwenye chanzo cha joto
kwenda kwenye sehemu yenye ubaridi. Nishati ya joto husafiri
katika vitu yabisi, vimiminika (vioevu na gesi) na nafasi tupu
(ombwe).
Jaribio namba 1: Kuchunguza joto linavyosafiri katika vitu
yabisi
Lengo: Kuonesha kusafiri kwa joto katika vitu yabisi
Mahitaji: Kipande cha metali au spoku, kipande cha
ubao, chanzo cha joto kama vile; jiko, kibiriti na
nta au mshumaa
Tahadhari: Chukua tahadhari wakati wote wa jaribio ili
kuepuka madhara ya moto.
79
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 79
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 79 14/01/2025 18:39