Page 92 - SayansiStd4
P. 92
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 4: Kukausha nguo kwenye jua
Matokeo
Kitambaa kikavu kilipowekwa katika maji kililowa. Kitambaa
kilicholowa kilipoanikwa juani kilikauka kutokana na joto
lililotokana na miale ya jua.
Hitimisho
Katika jaribio hilo tumejifunza kwamba kitambaa kibichi
kilikauka kutokana na joto la jua. Joto la jua husafiri kufikia
vitu kupitia nafasi tupu kwa njia ya mnururisho.
Katika majaribio uliyofanya, umegundua joto husafiri kwa njia
kuu tatu ambazo ni mpitisho, mnururisho na msafara.
(a) Mpitisho ni usafirishaji wa nishati ya joto katika vitu vigumu
kama vile metali.
(b) Msafara ni usafirishaji wa nishati ya joto katika vimiminika
kama vile vioevu na gesi.
85
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 85
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 85 14/01/2025 18:39