Page 130 - SayansiStd4
P. 130
4. Bainisha miundo ya rangi katika Kielelezo namba 17.
5. Chora picha ya nyumba kwa kutumia maumbo na mistari
katika programu ya Paint.
FOR ONLINE READING ONLY
Kuunda michezo sahili ya kompyuta
Uundaji wa michezo sahili ya kompyuta unahusisha uandikaji
wa maagizo kwa kutumia lugha ya programu. Miongoni mwa
vitu muhimu vya kuzingatia unapounda michezo sahili ya
kompyuta ni kama vile sheria za mchezo, muda wa kucheza,
ubunifu na zana za kuunda michezo. Fuata hatua zifuatazo
kuunda michezo sahili ya kompyuta:
1. Chagua aina ya mchezo: Amua aina ya mchezo unaotaka
kuunda, kama vile mchezo wa kujibu maswali, kukwepa
vikwazo au kumbukumbu.
2. Chagua zana za kuunda mchezo: Tumia zana ya Scratch
kuunda mchezo wako. Zana hii ina kiolesura rafiki na hutoa
maelekezo ya hatua kwa hatua.
3. Unda wahusika na mazingira: Unda wahusika wa mchezo
na mazingira wanayocheza ndani yake. Hii inaweza
kujumuisha kuchora picha au kutumia picha zilizopo tayari
kwa mfano ‘Sprite’ kwenye programu ya Scratch.
4. Andika sheria za mchezo: Andika sheria za mchezo na
jinsi wachezaji wanavyopaswa kucheza.
5. Kusimba: Andika maagizo kwa kutumia lugha ya programu
ya bloku ili kupata mchezo unaohitaji.
6. Jaribu kucheza na rekebisha: Cheza mchezo wako
ili kuona kama kuna makosa au maeneo yanayohitaji
kuboreshwa. Rekebisha makosa yote na boresha mchezo
wako.
123
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 123
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 123 14/01/2025 18:39