Page 133 - SayansiStd4
P. 133
Sehemu za ‘Scratch window’
‘Scratch window’ ina sehemu kuu nne. Sehemu hizo ni
eneo la kuandikia, bloku, jukwaa na orodha ya ‘Sprite’ kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 21.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 21: Sehemu za programu ya Scratch
(a) Eneo la kuandikia: Mahali ambapo unaandika au kujenga
programu yako kwa kuunganisha bloku mbalimbali.
(b) Bloku: Inawezesha kupata na kuchagua bloku za kujenga
programu yako.
(c) Jukwaa: Mahali ambapo mchezo huonekana.
(d) Orodha ya Sprite: Kiwakilishi kinachotumika katika
kuonesha jinsi mchezo unavyofanyika.
(e) Aikoni Sprite: Sehemu ya kuchagua ‘Sprite’
Kuunda michezo sahili ya kujongea
Scratch inaweza kutumika kuandaa michezo inayomfanya
Sprite kujongea jukwaani. Fuata hatua ambazo zimetolewa na
Kazi ya kufanya namba 6.
126
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 126
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 126 14/01/2025 18:39