Page 128 - SayansiStd4
P. 128
Kuchora na kuunganisha maumbo
Unaweza kuchora maumbo na kuunganisha ili kupata
umbo lingine. Kwa mfano, chora mistatili mingi na upange
ili kutengeneza ukuta wa matofali. Badala ya kuchora kila
FOR ONLINE READING ONLY
mstatili kwa kutumia zana ya mstatili, unaweza kuchora mmoja
kisha kuiga na kubandika mara nyingi ili kutengeneza mistatili
mingine. Unaweza kutumia rangi kutengeneza miundo kwenye
ukuta kama ilivyooneshwa katika Kazi ya kufanya namba 3.
Kazi ya kufanya namba 4: Kuchora ukuta wa matofali
wenye rangi tofauti tofauti
Hatua
1. Chagua zana ya mstatili kwa kubofya kwenye zana ya
pembenne ‘Rectangle’. Angalia Kielelezo namba 13.
Kielelezo namba 13: Kuchagua umbo la mstatili
2. Chora matofali na upangilie kwa kunyoosha kama ilivyo
kwenye Kielelezo namba 14.
Kielelezo namba 14: Tabaka la kwanza la ukuta
3. Paka rangi ya kijivu na njano kama ilivyo katika Kielelezo
namba 15.
121
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 121
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 121 14/01/2025 18:39